Magazetini: Merkel akubaliana na mkataba wa uhamiaji wa UN
22 Novemba 2018Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung likiandika kuhusu mjadala wa bajeti bungeni na hotuba ya kansela Merkel kuhusu uhamiaji linasema, Merkel angeweza kulipima vizuri kwa usawa wa manufaa na madhara yake suala hili, badala yake amejiweka katika kundi la mataifa ambayo yanaonekana kuwa yanapendelea tu haki za binadamu. Mhariri anaandika:
Hii ni kazi bure, kwa kuwa Merkel anafikiri yuko katika upande wa watu wanaotaka kufanya mema zaidi duniani na sio wa wale wenye hisia za uzalendo ambao wanafikiria wakati wote kuhusu mipaka ya nchi zao. Kifungu anachopenda kunukuu ni kifungu cha kwanza katika katiba , kwa kuwa nchi yoyote inayotumia nguvu dhidi ya raia wake inapaswa kuzuiwa kufanya hivyo.
Gazeti la Mannheimer Morgen likiandika kuhusiana na mkataba wa Umoja wa mataifa kuhusu wahamiaji linasema:
Wakati wahamiaji katika nchi nyingi wanakotoka wakitambua kuhusu masharti magumu yanayokumbana nayo, wasingejaribu kufika katika mataifa tajiri. Ushirikiano , na wakati huo huo misaada , ama pia idadi maalum ya wanaoruhusiwa kuingia ni suala linalotiliwa mkazo sana nchini Ujerumani. Kwa pamoja ama mmoja mmoja, pamoja na hayo maisha katika kila familia yanaonesha ushirikiano unasaidia.
Gazeti la Frankenpost linazungumzia kuhusu uhusiano kati ya rais Trump na viongozi wa Saudia. gazeti linaandika
Rais Trump amesisitiza kwamba Saudia ni mshirika muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi, pamoja na utawala wa Iran. Lakini kumbukeni kwamba Wamarekani waliwahi kuubeba utawala wa Shah Reza Pahlevi na kupuuza hasira za wananchi wa Iran waliochukizwa sana. Mhariri anaandika kwamba Wamarekani wanaweza kuwa washindwa , wakati utawala wa Riyadh utakapoangushwa katika mapinduzi.
Mpambano kati ya halmashauri ya Umoja wa Ulaya na serikali ya Italia ndio mada inayojadiliwa na mhariri wa gazeti la Landeszeitung. Mhariri anaadikika:
Mpambano huo unaonekana kuiingiza Ulaya katika mzozo wa muda mrefu. Lakini Umoja wa Ulaya hautaweza kushinda mpambano huo dhidi ya Italia. Italia yenye uchumi wa tatu mkubwa barani Ulaya ni kubwa mno kuweza kuokolewa. Umoja wa Ulaya unaonesha kwamba vyama vya Lega na Nyota tano vinataka kutumia suala hilo katika uchaguzi wa bunge la Ulaya. Wakifanikiwa kunyakua wingi katika bunge hilo, mradi wa Ulaya umekufa.
Mwandishi : Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Yusuf, Saumu