Magazetini: Juncker akutana na Trump
26 Julai 2018Mhariri wa gazeti la Mittelbayerische Zeitung la mjini Regensburg anazungumzia kuhusu mkutano kati ya rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker na rais wa Marekani Donald Trump. Mhariri anaandika:
"Trump kwa kweli hana mwelekeo wa kufanya mambo kwa haki, badala yake anataka kutamalaki. Kwa hiyo anajaribu, kuugawa Umoja wa Ulaya. Badala ya kufanya mikataba na mataifa makubwa ambayo yana uwezo sawa na Marekani , anajaribu kutafuta mikataba na mataifa madogo madogo, ambayo anaweza kuyapeleka vile anavyotaka. Na anatumia njia ya kutoa misaada na kuondoa ushuru."
Gazeti la Flensburger Tageblatt likizungumzia mada hiyo ya mkutano kati ya Trump na Juncker linaandika kwamba Donald Trump anatoa sifa kwa mkutano wa kilele wa G7 na washiriki wake, lakini anakataa kutia saini tamko la pamoja la mkutano huo. Mhariri anaandika:
"Ndio sababu Kim Jong Un amekuwa mwerevu , ambaye anawapenda watu wake, kwa kuwa mtu anapata kitisho ,akikumbuka kile kilichomtokea Gaddafi , aliyeuwawa baada ya nchi yake kushambuliwa kwa makombora ya NATO. Kwa kifupi , Trump kama muwamba ngoma anapenda kuvutia kwake. Na matokeo yake bila shaka ni Marekani kwanza. Lakini je hayo ndio maajabu pekee ya mtu huyu ama kuna mbinu nyingine zaidi?"
Kuhusiana na mada juu ya uamuzi wa mahakama juu ya utafiti wa vinasaba, mhariri wa gazeti la Landeszeitung la mjini Lueneburg anaandika:
"Mashine ya inayosaga unga kwa upande wa mahakama inasaga taratibu, lakini inaleta unga laini kabisa. Kwa muda wa miaka mitano watafiti walikuwa wahangaika na matokeo ya utafiti wao wa vinasaba kuhusiana na mimea. Mahakama ya Ulaya hatimaye imetoa hukumu , kwamba ubadilishaji wa vinasaba vya asili na kuingizwa vinasaba vya vigeni katika mmea ni mbinu tu za utafiti na sio utaratibu wa kilimo kinachoweza kutumika moja kwa moja."
Mhariri wa gazeti la Koelner Stadt-Anzeiger, kuhusiana na uamuzi wa mahakama ya juu ya utafiti wa vinasaba, anaandika:
"Watumiaji wanapaswa kufahamishwa vizuri zaidi juu ya mbinu za vinasaba, ili kwa karibu waweze kutoa maamuzi yao kuhusiana na kilimo hicho. Matumizi ya mazao yanatokana na utaalamu huo yaweze kuwa bora zaidi. Hatari inaweza kuepukwa. Na kwa hiyo hali ya matumizi ya mazao yaliyobadilishwa vinasaba haitakuwa na matatizo tena hata kwa watu wanaopendelea mbegu za asili."
Mhariri wa gazeti la Emder Zeitung anazungumzia kuhusu joto na mioto inayowaka misituni. Mhariri anandika:
"Suala moja liko wazi hapa, mhariri anaandika kwamba hali hiyo ya hewa itaendelea kuwa mbaya zaidi. Hii ni moja kati ya matokeo ya dunia yetuinayotumia mbinu nyingi za kiufundi. Imetuwi vigumu sana kuweza kuchukua hatua kutokana na hali kama hizo ambazo si za kawaida. Kila siku hususan katika siku za kazi, kila kitu kinakwenda kama kilivyo. Watu wanakuwa kama mashine katika hatua za uzalishaji, bila kujali , iwapo nje kuna lundo la barafu ama kuna uhaba wa maji. Utaratibu huu unatuonesha kwamba binadamu ni sehemu tu viumbe na licha ya kuwa na uwezo wa ufundi lakini hatuwezi kudhibiti uasili."
Sudi:
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri:Yusuf Saumu