1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazeti ya Ujerumani leo yameandika kuhusu kupeleka jeshi la nchi hiyo huko Lebanon.

14 Septemba 2006

Suala kuu lililotawala uhariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo ni kuhusu uamuzi wa serikali ya Ujerumani , katika suala la uwezekano wa kuchangia hadi wanajeshi 2,400 katika jeshi la umoja wa mataifa litakalotumwa kulinda pwani ya Lebanon. Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani umeandikwa na Herbert Peckmann.

https://p.dw.com/p/CHUv

Mhariri wa gazeti la Münchener Abendzeitung anaandika :

Uamuzi wa muungano mkuu unaounda serikali, ikiwa ni pamoja na wengi wa wabunge wa chama cha Green, ni sahihi na unaoonyesha msimamo thabit.

Ni nani kuliko kansela basi ambae amekuwa akielezea msimamo wa kutambuliwa kuwapo kwa taifa la Israel kama sehemu ya sera ya taifa, asingepata nafasi ya kujitoa , wakati Marekani, Lebanon na Israel kwa pamoja zilivyoomba msaada wa kijeshi.

Nae mhariri wa gazeti la Handelsblatt kutoka Düsseldorf anaeleza kuwa ; wengi wa wananchi wa Ujerumani wanapinga , kwamba kwa mara ya kwanza wanajeshi wa nchi hii wamepelekwa katika eneo la mashariki ya kati. Wengi wanaona hatari, kwamba wanajeshi hao wanajikuta kati ya mpaka walipo Hizbollah na majeshi ya Israel.

Nae Mhariri wa Main –Echo kutoka Aschaffenburg anazungumzia jukumu la Ujerumani katika kazi hiyo.

Mhariri anasema: Enzi za vita zimekwisha, Ujerumani sasa inajikuta katika zama za kisasa za kidemokrasia , na kujiamini katika medani ya kimataifa na inapaswa kuchukua wajibu huo.

Sambamba na hayo gazeti la Tageszeitung kutoka Berlin linadokeza kuwa: Inaonekana kwa uhakika kabisa kuwa hakuna mbadala wa kuwapo kwa operesheni ya kimataifa. Hii si rahisi kuelezeka hata hivyo.

Kwa kuwa pamoja na hali hiyo kuna madai ya vita vya ukandamizaji vinavyoweza kuhalalishwa hapa.

Kuhusiana na marekebisho yanayotarajiwa bungeni gazeti la Rhein-Neckar – Zeitung halioni matatizo: Linasema mchango wa Ujerumani pamoja na uzoefu mdogo, lakini wenye ujasiri mkubwa na wajibu kuielekea Israel , imeweza kupata kuungwa mkono kwa wingi katika bunge la Ujerumani.Iwapo Ujerumani pamoja na jeshi zima la umoja wa mataifa UNILIL kama wataweza kupata mfumo bora, wa kuimarisha hatua za kuleta amani, litakuwa ni jambo zuri.

Mhariri wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung anauona uamuzi huo wa baraza la mawaziri kuwa ni wa kimsingi kwa kuandika kuwa uamuzi wa kutuma jeshi la wanamaji huko, kutokana na Ujerumani kuidhinisha hatua hiyo kunaufanya wajibu wa kujiingiza kisiasa katika mashariki ya kati kuwa mkubwa zaidi.

Pia linaona gazeti la Ostsee-Zeitung kutoka Rostock , kuwa kwa hakika uwekaji wa jeshi hilo baina ya pande hizo zilizomo katika mzozo ambao unaonekana kutoweza kupatiwa ufumbuzi sio tena wa hatari.

Wakati mhariri wa gazeti la Die Zeit anauliza, kwanini jeshi la Ujerumani ni lazima lishiriki katika jeshi la umoja wa mataifa huko Lebanon, na kujibu:

Hapa kwa kweli sio kila kitu, lakini mtu yeyote bila sababu akikataa kazi kama hiyo, hana nafasi pia katika masuala ya kidiplomasia.