1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko Lindi: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 19

Salma Mkalibala31 Januari 2020

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko eneo la Lindi Tanzania yaongezeka na kufika 19. mpaka sasa wananchi waliokolewa ni 4,900 na Vijiji vilivyokumbwa na mafuriko vimeongezeka kutoka 6 hadi kufikia 16.

https://p.dw.com/p/3X661
Tansania Überflutungen in Lindi
Picha: Salma Mkalibala

Idadi ya watu waliofariki kwenye mafuriko yaliyotokea Mkoani Lindi nchini Tanzania, imeongezeka na kufikia 19 baada ya kupatikana kwa miili mingine katika operesheni ya uoakoaji inayoendelea, huku wananchi wakieleza kuhitaji msaada wa kibidamu kama chakula na mavazi mkoani humo. 

Akizungumza na waandishi wa Habari katika kambi ya muda ya shule ya Msingi Kipindimbi wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai, amesema juhudi za uokoaji zinaendelea lakini changamoto ni kwamba boti za uokoaji zinashindwa kufika baadhi ya maeneo kutokana na kuwepo kwa magogo na miti mikubwa inayopelekea Boti kushindwa kufika maeneo hayo.

Ngubiagai ameeleza idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kuwa miili mingine bado haijafanikiwa kuokolewa na mpaka sasa wananchi waliokolewa ni 4,900 na Vijiji vilivyokumbwa na mafuriko vimeongezeka kutoka sita hadi kufikia kumi na sita.

Baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye kambi hiyo ya muda wameiambia Dw kwamba wanakabiliwa na uhaba wa chakula na mavazi na kuiomba serikali kuongeza juhudi za kuwaokoa wananchi ambao bado wako kwenye maeneo hatarishi.

Zaidi ya wananchi 15,096 sawa na kaya 3,774 wameathirika
Zaidi ya wananchi 15,096 sawa na kaya 3,774 wameathirikaPicha: Salma Mkalibala

Akizungumzia changamoto iliyopo ya uhitaji wa msaada wa kibidanamu, Kubiagai amekiri kuwapo kwa uhaba wa chakula na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuwachangia wahanga. Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Kilwa amewatahadharisha wananchi ambao bado wako maeneo ya mabondeni kuondoka mara moja kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha.

Zaidi ya wananchi 15,096 sawa na kaya 3,774 wameathirika na mafuriko hayo wilayani Kilwa na wakazi wa wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale wamepoteza makaazi kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Lindi.