Maendeleo ya Kilimo, Burkinafaso
26 Machi 2013Lakini tokea miaka ya tisini Burkina Farso imekuwa inaongeza tija ya kilimo mara dufu. Burkina Faso imeweza kuongeza tija ya kilimo kutokana na mpango bora wa umwagiliaji maji mashambani.Na wataaalamu wanasema tija zaidi inatarajiwa katika miaka ijayo.
Mkulima mmoja Mando Adaye anatueleza juu ya utaratibu huo wa umwagiliaji wa mashamba. Amesema anaridhika na njia bora zinazotumika, ambazo zimerahisishwa "Naridhika na mtindo wa umwagiliaji.Kila kitu kimerahishishwa.Mtu anapaswa kutumia pampu mara moja tu ili kuyasukuma maji.Hapo awali nililazimika kusimamia muda wote. Lakini sasa natumia pampu mara moja na kuondoka kwenda kulala, Sasa naweza kumwagilia shamba usiku mzima."
Kutokana na njia hiyo ya kumwagilia maji shamba lake,mavuno yanakuwa makubwa hata wakati wa ukame.
Katika juhudi za kuongeza tija, wizara ya kilimo ya Burkina Faso pia inasaidia. Seydina Oumar Troure ndiye anaesimamia mradi wa umwagiliaji kutokea kwenye ofisi yake ya wizara ya kilimo mjini Ouagadougou."Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kuueneza mpango wa umwagiliaji wa mashamba"
Wakulima wadogo wadogo wanapatiwa vifaa vinavyolipiwa na serikali. Serikali inatoa ruzuku ya kufidia theluthi mbili ya gharama."
Serikali ya Burkina Faso inakusudia kutenga kiasi cha Euro milioni sita mnamo mwaka huu kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa mashamba. Mkurugenzi wa mradi huo Seydna Oumar Troure amesema yapo matumaini ya kuifanya Burrkina Faso iwe nchi ya kuuza mazao ya kilimo nje na kuweza kuingiza fedha nyingi.
Kwa mfano tunauza nyanya na vitunguu nchini Ghana,Nigeria na Ivory Coast.Na ikiwa tutaweza kuboresha ufundi wa umwagiliaji wa maji, naamini tutafanikiwa kuyatumia mawezkano yote tuliyonayo ili kuuza mazao fulani katika nchi za Afrika Magharibi na hata kwenye masoko ya kimataifa."
Kwa sasa ni asilimia tano tu ya ardhi ya kilimo nchini Burkina Faso inamwagiliwa maji. Mawezekano ni makubwa.Hayo ameyasema mwakilishi wa benki ya mandeleo ya Ujerumani, KfW Stephan Neu.
Burkina Faso inatekeleza sera ya kilimo cha mashamba madogo madogo.Hadi kufikia hatua ya umwagiliaji wa mashamba makubwa njia bado ni ndefu katika Burkina Faso.Yafaa kutilia maanani kwamba Burkina Faso ni nchi inayokabiliwa na kile kinachoitwa shinikizo la ardhi, kwa sababu idadi ya watu inaongezeka kwa asilimia 3.2 kila mwaka. Eneo la kilimo haliwezi kuongezeka kama jins ambayvo watu wangelipendelea.
Mwandishi:Hille,Peter
Tafsiri:Mtullya abdu.
Mhariri:Mohammed Khelef