1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMsumbiji

Maelfu ya watu waathiriwa na mafuriko Msumbiji

13 Februari 2023

Mkuu wa shirika la usimamizi wa majanga nchini Msumbiji, amesema jana kuwa watu elfu 37 wameathirika na mafuriko ya wiki hii.

https://p.dw.com/p/4NOmg
Mozambik Fischer
Picha: AP

Mvua kubwa zilizonyesha tangu Jumatano zimesababisha maelfu ya makazi kufurika katika eneo lililo karibu na mji mkuu Maputo. Akizungumza kupitia redio ya taifa, Luisa Meque amesema karibu watu 18,000 wamewekwa kwenye vituo vya mapokezi.

Watu wanne walifariki katika mafuriko hayo, na 13,000 waliokolewa. Shule kadhaa na vituo vya afya pia vilifurika. Kanda ya kusini mwa Afrika hivi sasa iko kwenye msimu wake wa vimbunga vya kiangazi, ambao kawaida hushuhudia dhoruba kali na mvua kubwa hadi mwezi Machi au Aprili.

Msumbiji imekumbwa na vimbunga vikali mara kadhaa katika miaka ya karibuni. Karibu mwaka mmoja uliyopita, watu 53 walikufa baada ya kimbunga Gombe kuipiga nchi hiyo.