1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiArmenia

Maelfu wakimbia Nagorno-Karabakh kwa kuhofia kushambuliwa

29 Septemba 2023

Zaidi ya nusu ya wakaazi wa Nagorno - Karabakh wamelikimbia jimbo hilo lililojitenga na ambalo hivi karibuni Azerbaijan imedai kulidhibiti kikamilifu.

https://p.dw.com/p/4WwBx
Wakimbizi kutoka jimbo la Nagorno-Karabakh wakiwasili katika kituo cha misaada ya kibinadamu kijiji cha Kornidzor.
Wakimbizi kutoka jimbo la Nagorno-Karabakh wakiwasili katika kituo cha misaada ya kibinadamu kijiji cha Kornidzor. Picha: Alexander Patrin/TASS/picture alliance

Inaripotiwa watu wa jamii ya Armenia walianza kuondoka Nagorno - Karakabakh kuanzia Jumapili na kufikia jana Alhamisi, zaidi ya watu 78,300- ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya idadi jumla ya watu 120,000 walikuwa wamehamia Armenia.

Kwa mujibu wa maafisa wa Armenia, watu zaidi wanaendelea kulikimbia jimbo hilo.

Mamlaka za Azerbaijan zimeahidi kuheshimu haki za watu wa jamii ya Armenia, japo makumi kwa maelfu ya wakaazi wa Nagorno -  Karakabh wamehama kwa kuhofia kushambuliwa.

Katika miongo mitatu ya migogoro kati ya nchi hizo mbili huku kila mmoja ikimshtumu mwingine kwa mashambulizi, mauaji na aina nyengine ya ukatili, mgogoro huo umewaacha watu katika pande zote mbili wakiishi kwa hofu.