1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Maelfu ya madaktari wa Uingereza waanza mgomo

13 Machi 2023

Madaktari wa hospitali nchini Uingereza wameanza mgomo wa siku tatu hii leo, ikiwa ni sehemu ya wimbi la karibuni la migomo nchini humo inayoshinikiza maboresho ya mazingira ya kazi na malipo.

https://p.dw.com/p/4Oc9b
Großbritannien | Streik in London
Picha: Kin Cheung/AP Photo/picture alliance

Mgomo huo pia utawajumuisha walimu, wafanyakazi wa treni na watumishi wa umma, katika wimbi la karibuni la migomo nchini humo. 

Madaktari wanasema miaka kadhaa ya nyongeza ya mishahara iliyo chini ya viwango vya mfumuko wa bei inamaanisha kimsingi wamekuwa na punguzo la asilimia 26 ya malipo tangu mwaka 2008.

Kuelekea mgomo huo, chama cha Madaktari cha Uingereza, BMA, kinachowakilisha matabibu hao, kilizindua kampeni ya matangazo kikidai kuwa madaktari wapya wanalipwa mishahara midogo kuliko wafanyakazi wa maduka ya kahawa.

Mgomo huo wa kile kinachoitwa 'madaktari wadogo', ambalo ni tabaka la madaktari wasio wataalamu waandamizi, lakini ambao wana uzoefu wa miongo kadhaa, ndiyo mrefu zaidi kuwahi kuitishwa nchini humo.