1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHungary

Maelfu wahudhuria misa ya Papa Francis mjini Budapest

30 Aprili 2023

Maelfu ya watu walikusanyika kwenya uwanja wa katikati ya mji mkuu wa Hungary, Budapest kuhudhuria misa iliyoongozwa na Papa Francis anaemaliza ziara ya siku nne nchini humo katika muktadha wa vita vya nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Qj32
Ungarn l Papst Franziskus in Budapest l heilige Messe auf dem Kossuth-Lajos-Platz
Picha: Tibor Illyes/MTI via AP/picture alliance

Kwa mujibu wa taarifa, waumini zaidi ya alfu 80 walihudhuria misa hiyo. Papa Francis anatarajiwa kutoa hotuba kwenye chuo kikuu binafsi cha kanisa katoliki baadae  leo kabla ya kumaliza rasmi ziara yake nchini Hungary.

Hapo awali Papa Francis alitahadharisha juu ya uovu wa hali ya kutojali huku akiwasalimu wakimbizi wa Ukraine. Licha ya maumivu ya goti yanayomlazimisha kutumia kiti cha magurudumu, Papa Francis alionekana kuwa na hali nzuri katika ziara hiyo ya 41 ya nchi za nje tangu kuanza kutumikia wadhifa wa kuliongoza kanisa hilo mnamo mwaka 2013.

Soma pia: Papa akutana na wahamiaji nchini Hungary

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban, amewapokea wakimbizi wa Ukraine tofauti na msimamo wake wa hapo awali wa kupinga wakimbizi.