Maelfu waandamana Tigray dhidi vikosi vya kigeni
23 Mei 2023Matangazo
Waandamanaji hao walioshuhudiwa katika miji mikubwa kama Mekele, Adigrat na Shire wameamuru pia kurejeshwa makwao kwa mamilioni ya watu waliolazimika kuondoka kufuatia mzozo wa jimbo la Tigray uliosababisha pia maelfu ya vifo.
Soma pia: Jeshi la kikanda lajiondoa mji wa kimkati wa Shire-Tigray
Kulingana na wafanyakazi wa mashirika ya kibinaadamu, vikosi vya Eritrea bado vimesalia katika ardhi ya Ethiopia. Serikali mjini Addis Ababa imekataa kuzungumzia suala hilo.
Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia na washirika wao kutoka nchi jirani ya Eritrea na wale wa mkoa wa Amhara walipambana na vikosi vya Tigray kwa miaka miwili, na vita hivyo vilihitimishwa kwa makubaliano yaliyofikiwa mwezi Novemba mwaka jana.