1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana kupinga mauwaji ya wanawake Kenya

28 Januari 2024

Maelfu ya watu wameandamana katika miji kadhaa nchini Kenya wakipinga mauaji dhidi ya wanawake.

https://p.dw.com/p/4blOe
Mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Wanaharakati wa haki za binadamu wakati wa maandamano ya kutaka kusitishwa kwa mauaji ya wanawake nchini humo.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Maandamano hayo ndiyo makubwa zaidi ya kupinga mauaji yanayotokana na ukatili wa kijinsia yaliyowahi kufanyika nchini humo.

Katika mji mkuu, Nairobi, waandamanaji waliosababisha kusimama kwa huduma za usafiri, walivalia fulana zenye majina ya wanawake waliouwawa mwezi huu.

Kulingana na mwandishi wa habari mwandishi wa habari Patricia Andago wa shirika la habari na utafiti la Odipo Dev aliyeshiriki pia katika maandamano hayo, takriban wanawake 14 wameuwawa kwa mwezi Januari mwaka huu pekee.

Visa viwili kati ya hivyo vilivyolitikisa taifa hilo mwezi huu, vilihusisha wanawake wawili waliouwawa katika makazi ya kukodi kwa muda.

Shirika la Odipo Dev liliripoti wiki hii kuwa, matukio katika habari yalionesha kuwa wanawake wasiopungua 500 waliuwawa kutokana na vitendo vya ukatili dhidi yao tangu Januari 2016 hadi Desemba 2023.