Maelezo juu ya mkutano wa chama cha CDU na Judith Hartl
29 Agosti 2005Hisia hizo pia zilitamalaki kwenye mkutano mkuu wa dharura wa chama cha bi Merkel uliofanyika mjini Dortmund.Mkutano huo wa jana ulijawa hisia za ushindi wa bi Merkel.Kila hatua ilipangwa kwa uthabiti wote.Palikuwa na muziki mtindo wa rock , palikuwa na dansa mithili ya Broadway.
Wanachama wa CDU , vijana kwa wazee walisheherekea kana kwamba bi Merkel tayari ameshapita katika uchaguzi.Nderemo hizo hazikutoa mwanya kwa masuala muhimu ya siasa kujadiliwa. Lakini ni wazi kwamba wajumbe walipata wasaa wa kutosha kuvikosoa vyama hasimu vya siasa na hasa cha Kansela Gerhard Schröder, SDP.
Mawaziri wakuu wote kutoka majimbo yanayotawaliwa na chama cha CDU walikuwapo kwenye mkutano huo kwa lengo la kutimiza jukumu moja muhimu sana; yaani kumwuunga mkono mjumbe wao bi Angela Merkel aliyeitwa Angie kwa huba katika siku zote tatu za mkutano huo.Na hata waziri mkuu wa jimbo la Bavaria bwana Edmund Stoiber alisisitiza utiifu na mshikamano na bi Merkel.
Hatahaivyo bi Merkel bado hajashinda uchaguzi. Hayo yatafahamika tarehe 18 mwezi ujao.Na ukweli ni kwamba ingwe inayoshikiliwa na chama cha bi Merkel siyo kubwa sana kama kura za maoni zinavyoonyesha.Kwa mujibu wa kura hizo chama hicho kipo mbele lakini siyo kwa hatua kubwa sana.
Vifijo vilivvokuwapo kwenye mkutano vilikuwa vikubwa mno. Mavazi ya wanachama na hata ya bi Merkel mwenyewe yalikuwa ya rangi za ushindi.Aliyetayarisha mkutano huo alifanya kazi yake bara bara.
Kampeni ya uchaguzi imepamba moto Jambo muhimu ni programu za chama zitakazovuta kura za wananchi. Uchaguzi wa safari hii hautakuwa rahisi kwa vyama vikuu yaani CDU na kinachotawala sasa cha Kansela Gerhard Schröder. Kwani tayari jumuiya nyingine yenye nguvu imejitokeza.
Chama cha bi Merkel kimeahidi kupunguza mzigo unaobebwa na waajiri.Ndio kusema waajiri watapunguziwa gharama kama vile kulipa mchango wa juu kwa ajili ya pensheni za wafanyakazi wao.
Lakini wakati huo huo .chama hicho kinasema kitaongeza kodi ya mauzo. Jee programu hiyo itawavutia wananchi na hasa watu wasiokuwa na ajira ? Ni kwa kiasi gani mkutano huo umesaidia katika kampeni ya bi Merkel kufanikiwa kuwa Kansela wa kwanza mwanamke katika historia ya Ujerumani?
.