MADRID.Waziri aingilia kati kupoza mvutano baina ya Venezuela na Uhispania
13 Novemba 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Uhispania bwana Moratinos ameingilia kati ili kupoza mvutano baina ya nchi yake na rais Hugo Chavez wa Venezuela.
Mvutano huo ulitokea kwenye mkutano uliofanyika nchini Chile mwishoni mwa wiki ambapo mfalme Juan Carlos wa Uhispania alimwambia rais Chavez afunge mdomo wake.
Mfalme Carlos alikasirishwa baada ya rais Chavez kumwita aliekuwa waziri mkuu wa Uhispania Aznar kuwa ni fashisti.
Waziri wa mambo ya nje wa Uhispania amesema mvutano huo asilani usiathiri uhusiano baina ya nchi yake na Venezuela na ameeleza kuwa nchi yake inataka mazungumzo yaendelee na Venezuela lakini katika msingi wa kuheshimiana.