1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID.Watuhumiwa 29 wafikishwa mahakamani kwa mauaji ya Madrid

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSA

Watuhumiwa 29 wamefikishwa mahakamani mjini Madrid nchini Uhispania kujibu tuhuma mashambulio ya mabomu ya mwaka 2004 dhidi ya treni yaliyowauwa watu 191 na kuwajeruhi watu wengine 2000.

Usalama unatarajiwa kuimarishwa katika maeneo ya mahakama ambapo watuhumiwa hao wenye asili ya Kiarabu na Kihispania wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na kundi la kigaidi na pia kuiba baruti kutoka kwenye machimbo ya kaskazini mwa Uhispania na kuwauzia baruti hizo watu wanaofanya mashambulio.

Uhispania imejiweka katika hali ya tahadhari dhidi ya mashambulio ya kigaidi wiki chache kabla ya kumbukumbu ya tatu ya mauaji ya kigaidi yaliyofanyika tarehe 11 mwezi Machi mwaka 2004.