MADRID:Mawaziri wa Ulaya kuzuru Lebanon
14 Oktoba 2007Matangazo
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Uhispania,Ufaransa na Italia wanazuru Lebanon wiki ijayo ikiwa ni juhudi za kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kisiasa nchini humo.Ziara hiyo inafanyika huku uchaguzi unasubiriwa na ina lengo la kuwaleta pamoja wanasiasa kwa madhumuni ya kupata maridhiano ya kitaifa.
Lebanon inakabiliwa na mkwamo wa kisiasa kwasababu vyama vya kisiasa vinashindwa kupata mrithi wa rais Emile Lahoud anayeungwa mkono na nchi jirani ya Syria.Muhula wa Rais Lahoud unakamilika mwezi Novemba huku Bunge likiahirishwa hadi tarehe 23 mwezi huu ili kuwapa wabunge muda zaidi wa kumtafuta rais mpya.Bunge la Lebanon halijafanya vikao vyovyote tangu Nomvemba mwaka jana.