MADRID:Kura ya ndio yategemewa Uhispania
20 Februari 2005Wananchi wa Uhispania leo wanapiga kura ikiwa ni kura ya maoni ya kwanza kabisa juu ya katiba mpya ya Umoja wa Ulaya ambapo wanaoiunga mkono katiba hiyo wanataraji Uhispania inayopendelea Umoja wa Ulaya itaonyesha mfano mzuri kwa wale wasiokuwa na misimamo katika umoja huo.
Waziri Mkuu Jose Luis Rodrigues Zapatero ameiweka hatarini hadhi yake kwa kuwafanya wananchi wa Uhispania ambayo imejiunga na Umoja wa Ulaya hapo mwaka 1986 kuwa mwanzo kuidhinisha katiba hiyo.
Kura ya Ndio inatarajiwa kupatikana kwa urahisi lakini kujitokeza kwa idadi ndogo ya wapiga kura kutakuwa pigo kwa Zapatero baada ya wapinzani kumshutumu kwa kuwaharakiza wananchi wake kupiga kura hiyo.
Nchi nyengine nane za Umoja wa Ulaya zinatarajiwa kuitisha kura hiyo ya maoni juu ya katiba ya Ulaya.Katiba hiyo mpya ya Umoja wa Ulaya inakusudia kuufanya umoja huo uendeshe shughuli zake kwa utulivu kufuatia kutanuka kwake na kuwa na nchi wanachama 25 hapo mwaka jana lazima iridhiwe na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya.