1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid: Zima moto wadhibiti moto visiwani Gran Canaria

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcx

Wakuu wa Uhispania wamesema zima moto wamefanikiwa kudhibiti moto uliokuwa ukiteketeza misitu na vichaka katika visiwa vya Gran Canaria.

Wakuu hao wamesema pia moto uliokuwa ukiteketea Tenerife umedhibitiwa.

Moto huo umekuwa ukiwaka tangu mwishoni mwa juma lililopita.

Kiasi wakazi elfu tano waliokuwa wamehamishwa kutoka makazi yao Gran Canaria, wamerejea majumbani mwao.

Waziri Mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero amevizuru visiwa hivyo ili ashuhudie hali halisi ilivyo.

Kiasi hekta elfu thelathini na tano zimeteketea ikiwemo thuluthi ya ardhi ya misitu visiwani humo.