MADRID: Zapatero ataka kukatiza mawasiliano na waasi wa kundi la ETA
31 Desemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Hispania, Jose Luis Rodriguez Zapatero, amesema anataka kusitisha juhudi za amani na waasi wa Basque wa kundi la ETA. Hatua hiyo inafuatia shambulio la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya motokaa lililofanywa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madrid.
Kundi la ETA linashukiwa kuhusika na shambulio hilo lililowaua watu takriban 19. Redio ya kitaifa ya Hispania iliripoti juu ya simu iliyopigwa na mtu alidai kwamba kundi la ETA lilifanya shambulio hilo.
Kundi hilo lilikuwa halijafanya shambulio lolote tangu lilipofikia makubaliano ya kusitisha uhasama na serikali mnamo mwezi Machi mwaka huu.