1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Wazimamoto wawili wauwawa na moto nchini Uhispania

8 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEn2

Moto unaoendelea kuwaka katika misitu nchini Uhispania umesababisha vifo vya wazima moto wawili, huku eneo la kusini mwa Ulaya likikumbwa na moto mkubwa. Uhispania, Ureno na sehemu za Ufaransa zimeathiriwa sana na moto.

Nchini Ureno wazima moto wanakabiliana na visa tofauti vya moto uliozuka katika maeneo mbalimbali, mingine inasemekana imewashwa makusudi. Nchini Ufaransa moto umesababisha kambi za mapumziko kuhamishwa na umeme kukatika katika nyumba yapata elfu 50.