Madrid: Wazima moto 11 wafariki Uhispania kutokana na moto mkubwa
19 Julai 2005Matangazo
Wazima moto 11 wa Uhispania wamekufa kutokana na moto mkubwa wa msituni unaowaka katikati ya nchi hiyo. Moto huo yaonesha ulisababishwa jumamosi iliopita na makaa yasiozimwa vizuri baada ya kufanwa karamu ya mishikaki.. Moto huo, ukisukumwa na pepo kali, ulienea katika mkoa wa GUADALJARA ulio na ukame, hivyo kuwalazimisha mamia ya watu wahame kutoka vijiji vyao. Wazima moto wanaendelea kupambana na moto huo hii leo, ikiwa ni siku ya tatu mfululizo.