1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID. Watu wajeruhiwa katika shambulio la bomu mjini Madrid.

25 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAC

Watu wasiopungua 34 wamejeruhiwa mapema leo katika mripuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya motokaa mjini Madrid, Uhispania. Maafisa wanasema waasi wa kundi la ETA wa chama cha Basque walionya kuhusu kufanya shambulio hilo mjini humo.

Waziri mkuu Jose Luis Rodrigeuz Zapatero amelilaani shambulio hilo, akilitaja kuwa kitendo cha kigaidi na kuwataka waaasi wa kundi hilo waweke silaha zao chini. Bomu hilo liliripuka dakika 45 baada ya gazeti la Basque kupokea onyo kutoka kwa kundi hilo la waasi.