Madrid. Watu 50 wafariki baharini.
7 Novemba 2007Matangazo
Hispania na Mauritania zimesema kuwa kiasi cha watu 50 kutoka bara la Afrika wamepatikana wamekufa katika bahari ya Atlantic baada ya kujaribu kusafiri kutoka Senegal kwenda katika visiwa vya Canary. Katika boti iliyowasafirisha, walinzi wa pwani wa Mauritania waliwapata watu 96 wanahimiaji kutoka Afrika wakiwa hai. Maafisa kutoka nchi hizo mbili wamesema kuwa kundi hilo la watu liliishiwa mafuta na kutumia kiasi cha wiki mbili wakielea baharini bila chakula.