MADRID: Washukiwa ugaidi wakamatwa Uhispania
21 Septemba 2007Matangazo
Raia 2 wa Pakistani wamekamatwa nchini Uhispania wakishukiwa kusaidia kifedha,vitendo vya ugaidi duniani.Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani imesema,washukiwa hao walikamatwa katika uvamizi uliofanywa kwenye miji ya Madrid na Barcelona.Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia operesheni ya ushirikiano ya miaka mitatu,kati ya polisi ya Uhispania na Shirika la Upelelezi la Marekani,FBI.