MADRID: Washukiwa 16 wakamatwa kwenye msako nchini Spain
16 Juni 2005Matangazo
Polisi nchini Spain wamewakamata watu 16 wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiislamu. Wizara ya ndani nchini humo imesema kwenye taarifa yake kwamba 11 kati ya washukiwa hao wanaaminika kuwa na mahusiano na kiongozi wa kigaidi wa mtandao wa Alqaeda nchini Iraq Abu Musab Al Zaqawi.
Washukiwa wengine watano wanahusishwa na mashambulio ya mabomu ya Marchi mwaka 2004 mjini Madrid ambapo watu 191 waliuwawa .
Washukiwa hao walikamatwa katika operesheni iliyofanywa na kikosi maalum cha polisi huko Madrid,Barcelona,Valencia na Cadiz.