MADRID: Waranti ya kuwakamata wanajeshi wa Marekani yatolewa
20 Oktoba 2005Matangazo
Jaji mmoja wa mahakama kuu nchini Uhispania ametoa waranti ya kukamatwa wanajeshi watatu wa Marekani kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mpiga picha za televisheni wa nchi hiyo wakati wa vita vya Irak.
Wanajeshi hao wanashtakiwa kwa kuhusika katika shambulio dhidi ya hoteli inayoitwa Palestina mjini Baghdad mwezi Aprili mwaka wa 2003. Hoteli hiyo ilikuwa ikitumiwa na waandishi habari wote wa kimataifa kwa wakati huo.
Marekani imewaondolea lawama wanajeshi hao ikisema hawana hatia, licha ya jeshi kukiri kwamba kombora moja lilivurumishwa katika hoteli hiyo kutoka kwa kifaru walimokuwa maofisa hao. Haijabainika wazi ikiwa wanajeshi hao watapelekwa nchini Uhispania.