1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid. Wapiganaji wanaotaka kujitenga wa kundi la ETA walipua mabomu dhidi ya kituo cha kuzalisha umeme.

13 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEv2

Kumetokea mashambulizi kadha ya mabomu karibu na kinu cha kuzalisha umeme kaskazini ya Hispania.

Kundi linalotaka kujitenga la Basque ETA limedai kuhusika na milipuko hiyo.

Maafisa wa Hispania wamesema kuwa wamepata taarifa za tahadhari , iliyotolewa na ETA nusu saa kabla ya milipuko.

Polisi waliwaondoa watu zaidi ya 200 kutoka katika kituo hicho cha umeme katika mji wa Basque wa Amorebieta na hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Wakati huo huo , katika tukio jingine mlipuko uliosababishwa na bomu lililotengenezwa kienyeji limemjeruhi polisi katika kituo cha kitamaduni cha Italia mjini Barcelona. Polisi wamesema kuwa mlipuko huo umesababishwa na kundi moja la Kitaliani linalopendelea ghasia.