Madrid. Wanajeshi watatu wa Marekani watakiwa kwa mashtaka nchini Hispania.
20 Oktoba 2005Jaji mmoja wa mahakama kuu nchini Hispania ametoa hati ya kukamatwa wanajeshi watatu wa Marekani kwa kuhusika na kifo cha mpiga picha za televisheni wa nchi hiyo wakati wa vita vya Iraq.
Wanajeshi hao watatu wanatuhumiwa kuwa walikuwamo katika kifaru ambacho kilifyatua kombora lililopiga hoteli inayojulikana kama palestina mjini Baghdad mnamo Aprili 2003.
Hoteli hiyo ilikuwa inatumiwa na karibu waandishi habari wote wa kimataifa kwa wakati huo.
Marekani imesema kuwa watu hao hawana hatia , licha ya kwamba jeshi limekiri kuwa kombora moja lilifyatuliwa kutoka katika kifaru hicho dhidi ya Hoteli hiyo.
Haifahamiki iwapo watu hao watatu wanaweza kupelekwa nchini Hispania.