1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid: Wakimbizi zaidi kutoka Afrika wawasili Spain na Italy.

3 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CBIN

Polisi wa Spain peke yake jana waliwakamata huko katika Visiwa vya Kanary wakimbizi 670 kutoka Afrika, idadi kubwa kabisa kwa siku moja. Si chini ya mashua nane zilikamatwa. Wakuu katika Visiwa vya Kanary wanasema hali ni ya hatari kutokana na kuengezeka sana idadi ya wakimbizi hao wanaokuja kwa njia isiokuwa ya kisheria. Wameutaka Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa zisaidie.

Huko Sicily kikundi cha wakimbizi 19 kutokea Eritrea waliokolewa. Inasemakana walikuwa siku kumi na mbili njiani baharini. Wenziwao wanane walikufa njiani.