MADRID: Wakimbizi waendelea kumiminika Hispania
1 Agosti 2006Matangazo
Hakuna ishara ya kupunguka ule mmiminiko wa wakimbizi wa Kiafrika katika Visiwa vya Kanary vya Hispania.Kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo, tangu siku Jumapili,zaidi ya Waafrika 200 waliokuwa katika boti nne walitua kwenye visiwa hivyo.Wakati huo huo,maiti za wanaume 12 zimekutikana pwani,kaskazini mwa mji mkuu wa Senegal,Dakar.Haijulikani kama watu hao pia walijaribu kukimbilia Ulaya kwa boti,kwa njia isiyo halali.Senegal na nchi jirani,Mauretania mara kwa mara hutumiwa na wakimbizi wa Kiafrika kama kituo cha safari ya kuelekea Visiwa vya Kanary.