Madrid. Wahispania mashoga ruksa sasa kuoana.
1 Julai 2005Matangazo
Bunge la Hispania limepitisha sheria inayoruhusu watu wa jinsia moja kuoana na kupata haki ya kuwatunza watoto wa kupanga. Muswada huo ambao ulikataliwa kwanza na baraza la seneti la nchi hiyo wiki iliyopita sasa utakuwa sheria kutokana na kukubaliwa na bunge.
Sheria hiyo mpya itaanza kazi katika muda wa mwezi mmoja.
Hatua hiyo inaifanya Spain kuwa nchi ya tatu kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja , baada ya Uholanzi na Ubelgiji kufanya hivyo.
Bunge la Canada lilipitisha sheria kama hiyo mapema wiki hii, lakini bado inahitaji kupitisha na baraza la nchi hiyo la seneti.