1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid: Wahamiaji kutoka Afrika magharibi wazama

28 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoi

Redio ya Uhispania imeripoti kwamba watu wapatao 10- wahamiaji waliojaribu kuingia nchini humo wakitokea Afrika magharibi wamezama baada ya Jahazi yao kupinduka. Wengi wengine wanaripotiwa wamepotea. Jahazi hiyo ilitokea Sahara magharibi ikielekea katika visiwa vya karibu vya Canary vinavyo tawaliwa na Uhispania. Bado kuna ripoti za kutatanisha juu ya idadi hasa ya waliokuwemo ndani ya chombo hicho. Karibu watu 300 wamekufa mwaka huu,wakati wakijaribu kufuka Sahara magharibi kuelekea visiwa vya Canary.