Madrid. Waandamana dhidi ya kushusha hadhi ya masomo.
13 Novemba 2005Matangazo
Mamia kwa maelfu ya Wahispania wamefanya maandamano mjini Madrid wakipinga dhidi ya kushusha hadhi ya masomo ya dini katika shule.
Chini ya sheria mpya ya elimu , haitakuwa tena lazima kuchukua masomo ya dini, hata katika shule kibinafsi zinazopewa msaada na serikali zinazoendeshwa na kanisa Katoliki.
Wengi wa waandamanaji hao ni kutoka katika kanisa lenye nguvu nchini Hispania la Katoliki, ikiwa hii ni mara ya kwanza kwa kanisa kusuguana na serikali inayoongozwa na chama cha Kisoshalist.