MADRID: Waafrika 50 wasakwa baharini Ulaya
19 Julai 2007Matangazo
Walinzi wa pwani nchini Hispania,wanawasaka kiasi ya Waafrika 50 waliokuwa katika boti iliyopinduka baharini.Watu hao walitaka kukimbilia Visiwa vya Kanary kwa njia zisizo halali.Waafrika wengine 48 wameokolewa baharini,kama maili 89 kusini-magharibi ya kisiwa cha kitalii cha Tenerife.