MADRID : Uhispania yapiga kura juu ya katiba ya Ulaya
20 Februari 2005Matangazo
Wananchi wa Uhispania leo wanapiga kura ya maoni juu ya katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.
Uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba kuna matarajio ya kura ya ndio lakini kuna wasi wasi pia kwamba watu watakaojitokeza kupia kura hiyo watakuwa ni wachache.Nchi nyengine 10 za Umoja wa Ulaya zinatazamiwa kuitisha kura hiyo ya maoni juu ya katiba ya Umoja wa Ulaya.
Wakati huo huo Ureno leo inapiga kura ambapo chama cha Kisoshalisti kinatazamiwa kushinda kufuatia kampeni yake iliokita juu ya utulivu na ukuaji wa uchumi katika nchi hiyo ya kimaskni kabisa Barani Ulaya.