1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid: Syria inasema itajiingiza Lebanon pindi majeshi ya Israel yataukaribia mpaka wan chi yake.

23 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG4n

Syria itajiingiza katika mzozo kati ya Israel na Chama cha Hizbullah cha Lebanon pale majeshi ya nchi kavu ya Israel yatakapoingia Lebanon na kuukaribia mpaka wa Syria. Hayo yalitamkwa na waziri wa habari wa Syria, Mosen Bilal, kwa gazeti la Uhispania la ABC. Wakati huo huo, Bwana Bilal alisema hiyo haina maana Syria inasaidia katika mzozo huo.

Kwa upande mwengine, juhudi zinaendelea za kuutanzua mzozo huo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Steinmeier amekutana na waziri wa ulinzi wa Israel, Perez. Bwana Perez alisema Israel iko tayari kukubali jeshi la kimataifa liwekwe Kusini mwa Lebanon. Ndani ya ratiba ya waziri Steinmeier amepangiwa akutane na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, na rais wa Wapalastina, Mahmud Abbas. Hapo kabla alipokuweko Misri ambako alifanya mazungumzo na waziri mwenzake, Ahmed Abul Gheit, Bwana Steinmeier alisema:

Na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, ameionya Israel isiivamie Lebanon:

+Nafikiri jambo hilo litakuwa la hatari sana kuupabnua mzozo huo. Bila ya shaka yatazidi mapigano baina yao na Hizbullah. Ikiwa watabaki huko na kukusudia kile walichokiita hao zamani ukanda wa amani, huo utakuwa ukanda wa amani kwao, lakini kwa wengine itamaanisha ardhi yao imetekwa. Na jambo hilo litazidisha upinzani.+

Pia waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Bibi Condoleezza Rice anatazamiwa kuwasili katika eneo hilo la mzozo, licha ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Philippe Douste-Blazy, na waziri wa nchi katika wizara ya mambo ya kigeni ya Uengereza kuhusu Mashariki ya Kati, Kim Howell. Bwana Howell alisema serekali ya nchi yake inaanza kuhoji juu ya mbinu zinazotumiwa na Israel.

Na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani mjini Berlin imetoa ilani kwamba raia wa Kijerumani na wa nchi nyingine za Umoja wa Ulaya ambao bado wako Kusini mwa Lebanon wanaweza kesho kusafirishwa kwa meli iliokodiwa kutokea Lebanon kwenda Cyprus. Na kutoka hapo tayari ziko ndege za kuwasafirisha hadi nchi zao. Watu hao wanatakiwa wakusanyike katika nyumba ya mapumziko huko Tyrus, Sur.