MADRID : Sheria ya kutowa mimba kuidhinishwa
12 Februari 2007Waziri Mkuu wa Ureno Jose Socrates ameahidi kupitisha sheria ya kuhalalisha utowaji wa mimba baada ya wapiga kura kuunga mkono hatua hiyo katika kura ya maoni.
Juu ya kwamba idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika kura hiyo ya maoni ilikuwa sio ya kutosha kushurutiusha iwe sheria Soctares amesema matokeo yake yameonyesha wazi kwamba wananchi wa Ureno wanataka sheria juu ya utowaji mimba ibadilishwe.Matokeo rasmi ya mwisho yameonyesha kwamba takriban asilimia 60 ya wapiga kura wameidhinisha pendekezo la serikali kuwapa wanawake wote haki ya kutowa mimba ya ujauzito wa hadi wiki 10.
Ureno ambalo kwa kiasi kikubwa ni taifa la madhehebu ya Kikatoliki ina sheria kali kabisa za utowaji mimba miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.