MADRID: Rais Hu Jintao ziarani Hispania
14 Novemba 2005Matangazo
Rais Hu Jintao wa China akiwa katika sehemu ya mwisho ya ziara yake barani Ulaya amewasili nchini Hispania.Wanaharakati walikusanyika mbele ya ubalozi wa China mjini Madrid wakilalamika kuhusu haki za binadamu nchini China.Mikutano rasmi ya Rais Hu wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini Hispania,inaanza hii leo.Atakutana pia na Mfalme Juan Carlos na waziri mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero wa Hispania.Kabla ya kwenda Hispania,Rais Hu alikuwepo Ujerumani kwa ziara ya siku tatu. Wakati wa ziara hiyo alikutana na viongozi wa Ujerumani na alitia saini mikataba kadhaa ya kibishara.