1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Polisi wakamata vifaa vya kutengezea silaha

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDW

Polisi nchini Uhispania wamegundua kiwango kikubwa cha vifaa vinavyoweza kuripuka katika eneo la kaskazini la nchi hiyo. Ugunduzi huo ni wa pili katika kipindi cha siku nne.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uhispania imesema katika taarifa yake kwamba polisi walikamata takriban kilo 140 ya nyenzo zinazotumiwa kutengeza mabomu katika mkoa wa Navarra kazkani mwa nchi hiyo wakati wa operesheni dhidi ya waasi wa kundi la ETA la chama cha Basque.

Washukiwa wanane wametiwa mbaroni kuhusiana na operesheni hiyo iliyoanza Jumatano iliyopita.

Kundi la ETA linalaumiwa kwa vifo zaidi ya 800 katika kampeni yake ya miaka 38 kutaka uhuru wa eneo la Basque. Umoja wa Ulaya na Marekani inalitambua kundi la ETA kama kundi la kigaidi.