1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid. Polisi wakamata silaha kibao.

24 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgY

Polisi kaskazini mwa Hispania wamesema kuwa wamegundua silaha nyingi ambazo zinadaiwa kuwa mali ya kundi linalotaka kujitenga katika jimbo la Basque la ETA.

Maafisa wamegundua kilogram 50 za mada ya kemikali pamoja na vifaa vya kulipulia karibu na mji wa Basque ulioko kaskazini wa Amorebieta. Mapema wiki hii, waziri wa mambo ya ndani wa Hispania Alfredo Perez Rubalcaba ameieleza hatua ya kuleta amani na ETA kuwa iko katika bunge.