MADRID: Mshukiwa wa sita akamatwa kwa mashambulio ya kigaidi ya mwaka 2004.
5 Januari 2007Matangazo
Polisi wa Uhispania wamemtia nguvuni mshukiwa wa sita kwa kuhusika na mashambulio ya mwaka 2004 dhidi ya magari moshi mjini Madrid.
Mshukiwa huyo amekamatwa baada ya watu wengine watano kukamatwa mapema juma hili kwa tuhuma za kuwasaidia washukiwa wawili wa mashambulio hayo kutoroka.
Kwengineko, polisi wa eneo la Basque wamegundua bomu lililoachwa ndani ya gari katika mji wa Bilbao.
Msemaji wa polisi amesema gari hilo lilikuwa na baruti zenye uzito wa kilogramu mia moja.
Kundi la ETA linawania jimbo la Basque kujitenga liliuvuruga mwafaka wa amani kati yake na serikali jumamosi iliyopita baada ya kuripua bomu katika uwanja wa ndege, mjini Madrid.