1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Mkutano kujadili tatizo la wakimbizi

2 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDG3

Hispania imeitisha mkutano wa kimataifa pamoja na nchi za Ulaya za eneo la Bahari ya Mediterania,kujadili tatizo la wahamiaji wa Kiafrika wanaojaribu kuingia Ulaya kwa njia zisizo halali.Naibu waziri mkuu wa Hispania,Maria Teresa Fernandez amesema,jumuiya ya Ulaya inapaswa kulishughulikia zaidi tatizo hilo.Siku ya Ijumaa peke yake,wakimbizi 430 kutoka Afrika walifika kwa boti kwenye Visiwa vya Kanary.Mwaka huu kama wakimbizi 19,000 kwenye boti wametua kwenye visiwa vya Kanary.Kwa mujibu wa mashirika ya misaada kiasi ya watu 3,000 wamepoteza maisha yao wakati wa kufanya safari ya hatari katika boti.