Madrid. Mamia waandamana kupinga sera kuelekea ETA.
11 Machi 2007Mamia kwa maelfu ya watu wameshiriki katika maandamano ya upinzani mjini Madrid wakipinga sera za serikali ya Hispania kuelekea kundi linalotaka kujitenga la ETA.
Waandamanaji wamekasirishwa na uamuzi wa serikali wa kulegeza masharti kwa wafungwa wa ETA, ambao ni wagonjwa baada ya kufanya mgomo wa kula.
Wanadai kujiuzulu kwa waziri mkuu kutoka chama cha Kisoshalist Jose Luis Rodriguez Zapatero.Chama cha upinzani cha Popular kinadai kuwa serikali imesalim amri kwa ETA. Serikali imesitisha hatua za kuleta amani baada ya ETA kuvunja makubaliano ya kusitisha uhasama yaliyodumu kwa muda wa miezi tisa kwa kufanya shambulio la bomu katika uwanja wa ndege wa Madrid Desemba mwaka jana.