Madrid. Mahakama kutoa hukumu leo.
31 Oktoba 2007Mahakama inayopambana na ugaidi nchini Hispania inatarajiwa kutoa hukumu leo dhidi ya watuhumiwa 28 wanaotuhumiwa kuhusika katika shambulio la bomu mwaka 2004 mjini Madrid shambulio ambalo limesababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Kila mmoja anakabiliwa na kifungo cha miaka 40 jela. Shambulio hilo la magaidi lilikuwa baya kabisa kuwahi kutokea tangu shambulio la Septemba 11 nchini Marekani. Wale waliohusika wanakana kuwa na uhusiano na Waislamu wenye imani kali ama kundi la al-Qaeda. Kundi la kigaidi lilitoa video siku mbili baada ya shambulio hilo, wakidai kuhusika . Watuhumiwa saba wa ugaidi walijilipua wiki tatu baada ya shambulio hilo walipokuwa wamezingirwa na polisi.