MADRID : Mabomu manne yaripuka karibu na mtambo wa umeme
13 Julai 2005Matangazo
Kumekuwepo na mfululizo wa miripuko karibu na mtambo wa kuzalisha umeme kaskazini mwa Uhispania.
Kitengo cha wapiganaji wa Basque wanaotaka kujitenga cha kundi la ETA kimedai kuhusika na miripuko hiyo.Mtu asiyejulikana alipiga simu na kutowa onyo nusu saa kabla ya kuripuka kwa mabomu hayo.
Polisi iliwahamisha zaidi ya wafanyakazi 200 kutoka mtambo huo ulioko katika mji wa Basque wa Amorebieta na hakuna mtu aliyejeruhiwa.