1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Kundi la ETA lasema bado linataka amani

9 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBD

Kundi la ETA la chama cha Basque limesema bado linawajibika kuhusu amani ili mradi serikali ya Uhispania itakomesha kile linachokiita mashambulio dhidi ya taifa la Basque.

Katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la Gara katika eneo la Basque, kundi la ETA limeonya huenda likaachana na mapambano yake ya kutumia silaha kupigania uhuru kaskazini mwa Uhispania kwa mujibu wa masharti yaliyopo kwa sasa.

Kundi hilo limesema linaheshimu tangazo lake la kusitisha mapigano la mwezi Machi mwaka jana ingawa lilivurugwa na shambulio la bomu dhidi ya uwanja wa ndege wa mjini Madrid mwezi Disemba. Maafisa wa serikali wamenukuliwa wakisema wanatarajia kundi la ETA litangaze kukomesha machafuko.

Kundi hilo limekuwa likiendeleza kampeni ya miaka 38 likipigania uhuru wa eneo la Basque ambayo imesababisha vifo zaidi ya 800.