1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID. Kesi ya ugaidi yaanza nchini Uhispania.

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKT

Watu watatu wamefikishwa mbele ya mahakama maalum mjini Madrid, Uhispania kujibu mashtaka ya kusaidia kupanga shambulizi la kigaidi la septemba 11 mwaka wa 2001 nchini Marekani.

Kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa inawahusisha aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda nchini Uhispania na watu wengine 23 ambao ni baadhi ya watuhumiwa katika kesi hii.

Kesi hii ni ya kwanza kuanza kusikilizwa katika mahakama iliyo jengwa upya katika jumba lenye udhibiti wa hali ya juu wa kiusalama nchini Uhispania ambako watuhumiwa watakaa kwenye kijichumba maalum cha kioo ambacho kina uwezo wa kuzuia risasi.

Katika kesi hii kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden pia ameorodheshwa kama mshtakiwa lakini kwa mujibu wa sheria za Uhispania kesi haiwezi kuendelea mahakamani iwapo mshtakiwa hayuko.