1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Kesi ya mashambulio ya treni yaendelea Hispania

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRh

Kesi ya watuhumiwa 29 wanaoshtakiwa kuhusika na mashambulizi ya mabomu kwenye treni inaendelea hii leo kwa siku ya pili katika mji mkuu wa Hispania,Madrid.Katika siku ya kwanza ya kesi hiyo,Mmisri Rabei Osman el-Sayed,mmojawapo anaeshtakiwa kuwa miongoni mwa wahusika 7 wakuu amekanusha mashtaka yote.Hadi mwezi wa Oktoba mahakama inatazamia kufikia uamuzi wake.Ikiwa kesi hiyo itaendelea baada ya muda huo,mahakama italazimika kuwaachilia huru baadhi ya washtakiwa,kwani kisheria washukiwa wanaweza kuwekwa kizuizini hadi miaka minne tu.Katika mashambulio hayo ya treni,hapo Machi mwaka 2004, watu 191 waliuawa na zaidi ya 1800 wengine walijeruhiwa.