MADRID :Kesi ya kuripua treni yaanza
15 Februari 2007Watu 29 wanafikishwa mahkamani leo hii nchini Uhispania kwa mashtaka juu ya kuripuwa treni kwa mabomu mjini Madrid hapo mwaka 2004 kulikouwa watu 191.
Uhispania imeimarisha tahadhari yake ya usalama kwa kuiweka katika kiwango cha kati kutoka kiwango cha chini wakati kesi hiyo ikianza ikiwa ni wiki chache tu kabla ya kumbumbuku ya miaka mitatu tokea mashambulizi hayo mabaya kabisa barani Ulaya yaliohusishwa na kundi la Al Qaeda.
Mamia ya polisi wanaweka ulinzi katika mahkama ya Madrid ambapo watuhumiwa Waarabu na Wahispania wanakabiliwa na mashtaka kuanzia kuwa wanachama wa kundi la kigaidi hadi kuiba baruti kwenye migodi ya kaskazini na kuwauziya wahusika wa mashambulizi hayo.
Mabomu hayo yalioripuka kwenye treni nne zilizosheheni abiria mbali na kuuwa watu 191 yamejeruhi wengine takriban 2,000.