1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid. Joto kali laikumba eneo la kusini mwa Ulaya.

20 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEsa

Eneo la kusini mwa Ulaya , likiwa katika hali ya joto kali , liko katika hali ya tahadhari baada ya moto kuteketeza sehemu kadha za Hispania, Ureno na Itali, na kusababisha vifo vya watu 12 na kuharibu maelfu ya hekta ya vichaka na misitu.

Hispania ndio iliyokumbwa na athari kubwa , na ambayo inakabiliwa kwa hivi sasa na ukame ambao haujapata kuonekana tangu mwaka 1945.

Moto katika misitu uliteketeza hekta 13,000 siku ya Jumamosi na kusababisha watu 11 waliokuwa wakijitolea kuuzima moto kufariki katika jimbo la kati la Guadalajara.

Moto huo ambao unaaminika kuwa umeanzishwa na watu waliokuwa wako katika mapumziko ya makambi wakichoma nyama , ulidhibitiwa leo Jumatano baada ya kupamba usiku na mchana.

Moto huo ulikuwa bado unawaka hadi hii leo mchana lakini umezungushiwa mpaka wa kilometa nane.