1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid. Hukumu yatolewa, jela miaka 40 kwa watuhumiwa.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Av

Mahakama inayowahukumu watuhumiwa wa ugaidi nchini Hispania imetoa hukumu kwa washtakiwa 21 wanaoshtakiwa kwa kuhusika na shambulio la bomu dhidi ya vituo vya treni nchini Hispania mwaka 2004. Jaji anayeendesha kesi hiyo amewapata na hatia watuhumiwa hao katika mashtaka kadha, ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi. Watuhumiwa watatu wamepewa kifungo cha zaidi ya miaka 30, lakini chini ya sheria za Hispania hukumu hiyo inaishia katika muda wa miaka 40 jela.

Waziri mkuu wa Hispania ameisifu hukumu hiyo na kusema imetimiza matarajio ya watu.

Mtu aliyefikiriwa kuwa kiongozi wa operesheni hiyo, Rabei Osman raia wa Misr , hakupatikana na hatia. Watu 191 wameuwawa na zaidi ya 2,000 wamejeruhiwa katika mfululizo wa mabomu ambayo yalilenga muda ambao watu wengi wanasafiri kwa treni asubuhi March 11, 2004 katika tukio baya kabisa la ugaidi katika ardhi ya Ulaya.